• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO: Maambukizi mapya ya Ebola yaripotiwa DRC

    (GMT+08:00) 2018-08-02 09:24:57

    Shirika la Afya Duniani WHO limesema, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imetangaza kuwa matukio mapya ya maambukizi ya homa ya Ebola yameripotiwa nchini humo, siku chache baada ya kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa homa hiyo magharibi mwa nchi hiyo.

    Serikali ya DRC imesema, matokeo ya upimaji yamethibitisha matukio mapya ya maambukizi ya Ebola katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ambayo yamekuja wiki moja baada ya wizara ya afya kutangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola mkoani Equateur.

    Idara ya afya ya huko imesema, nne kati ya sampuli sita zimethibitishwa kuwa na virusi vya Ebola katika taasisi ya taifa ya utafiti wa kimatibabu INRB huko Kinshasa. Upimaji zaidi unaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako