• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu ya Marekani yasema wito wa Trump kumaliza uchunguzi wa Russia sio amri

    (GMT+08:00) 2018-08-02 09:25:20

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema, kauli ya rais Donald Trump aliyotoa mapema jana kwenye ukurasa wake wa Twitter ya kumtaka mwanasheria mkuu Bw. Jeff Sessions kufunga uchunguzi unaoendelea kuhusu Russia kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016, ni maoni yake, na wala si amri.

    Bibi Sanders amesema hayo saa kadhaa baada ya rais Trump kutoa taarifa ikisema, Bw. Sessions anatakiwa kusimamisha uchunguzi unaoongozwa na mchunguzi maalumu Bw. Robert Mueller, hali inayoashiria kupamba moto kwa mashambulizi yake dhidi ya uchunguzi huo, na kuleta kizaazaa kuhusu lengo lake.

    Bibi Sanders amesema hiyo si amri, ni maoni binafsi ya rais, huku akiongeza kuwa rais anataka kuona mchakato huo unamalizika, kama alivyosema mara nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako