• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yaanza kurefusha reli ya SGR Kenya

    (GMT+08:00) 2018-08-02 10:10:45

    Kazi ya kurefusha reli ya SGR kutoka Nairobi hadi Naivasha imeanza kufanywa na kampuni ya ujenzi wa mawasiliano ya China (CCCC) .

    Kwa mujibu wa kampuni hiyo mradi huo umeanza katika kaunti ya Rift Valley, Narok. Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 120 ni moja ya sehemu tatu za mchakato wa pili wa mradi wa ujenzi wa reli ya SGR, ambayo itarefushwa hadi wilaya ya Malaba, iliyoko kwenye mpaka kati ya Kenya na Uganda.

    Msemaji wa mradi wa reli ya SGR wa kampuni hiyo Bw. Steve Zhao, amesema hivi sasa ujenzi wa vituo vya reli pia umeanza katika wilaya za Ongata Rongai, Ngong na Suswa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako