• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga soko lenye muundo kamili la matumizi ya fedha

    (GMT+08:00) 2018-08-02 18:06:59

    Katika nusu ya kwanza mwaka huu, idadi ya watazamaji wa filamu nchini China imezidi milioni 900, ongezeko la thamani ya mauzo ya rejareja kupitia mtandao wa Internet limezidi asilimia 30, wastani wa matumizi ya fedha katika michezo na mazoezi ya kujenga afya umeongezeka kwa asilimia 40, takwimu hizo zimeonesha kuwa matumizi ya fedha yamekuwa msukumo mkubwa wa kwanza katika kuhimiza ongezeko la uchumi nchini China. Ofisa wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China amesema, matumizi ya fedha ya wananchi wa China yanadumisha ongezeko kwa hatua madhubuti, na China itajenga soko lenye muundo kamili la matumizi ya fedha ili kuhimiza ongezeko jipya katika matumizi ya fedha.

    Takwimu zimeonesha kuwa, katika nusu ya kwanza mwaka huu thamani ya jumla ya mauzo ya rejareja imefikia yuan trilioni 18, hili ni ongezeko la asilimia 9.4 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na kuwa msukumo muhimu wa ongezeko a uchumi. Msimamizi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Liu Yunan ameeleza kuwa, ili kuhimiza zaidi matumizi ya fedha ya wananchi, China itajenga soko lenye muundo kamili wa matumizi ya fedha. Anasema:

    "Lengo la hatua hiyo ni kuondoa vizuizi vya kimuundo na kukidhi mahitaji ya matumizi ya fedha ya wananchi katika ngazi mbalimbali, kuandaa soko la matumizi ya fedha katika kiwango cha katikati na cha juu, ili kuhimiza ongezeko jipya la matumizi ya fedha."

    Kamati hiyo pia itakamilisha upimaji wa ubora na utaratibu wa utoaji wa mkopo, ili kuandaa mazingira yenye usalama ya matumizi ya fedha na kuboresha uwezo na makadirio ya matumizi ya fedha ya wananchi. Hivi sasa kadiri mapato ya wananchi na utoaji wa bidhaa zinavyoongezeka, ndivyo kiwango cha matumizi ya fedha ya wananchi kinavyoongezeka kwa kasi. Bw. Liu Yunan ameeleza kuwa katika kipindi kijacho China itafanya juhudi kuongeza utoaji wa bidhaa zenye kiwango cha juu na huduma zinazohusika. Anasema:

    "Tutazidi kulegeza masharti ya uidhinishaji katika sekta ya utoaji wa huduma, kuelekeza makundi ya umma kujiunga na nyanja muhimu za utoaji wa huduma na matumizi ya fedha zikiwemo utalii, utamaduni, michezo, afya, matunzo ya wazee, mafunzo na elimu, na kutoa msaada kwa makundi hayo na soko kutoa huduma zenye kiwango cha juu zaidi."

    Mbali na hayo kamati ya maendeleo na mageuzi ya China pia itaharakisha hatua ya kuinua kiwango cha matumizi ya fedha vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako