• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbinu za Marekani hazitafanya kazi kwa China

    (GMT+08:00) 2018-08-02 20:08:02

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China leo amesema kuwa, hatua zinazochukuliwa na Marekani hivi karibuni hazitaweza kuishawishi China.

    Amesema Marekani imetoa taarifa ya kuongeza ushuru wa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 kutoka 10% hadi 25%, na kwa upande mwingine, imesema itarejesha mazungumzo na China.

    Msemaji huyu amesema, kwa kufanya hivyo Marekani haitilii maanani maslahi ya dunia na ya wakulima, wafanyabiashara na wateja wake. Kitendo hicho hakitafanya kazi kwa China, pia kitasikitisha nchi na sehemu zinazopinga vita ya biashara. Amesisitiza kuwa, China imefanya maandalizi ya lazima kukabiliana na hatua hizo za Marekani, ili kulinda heshima ya nchi na maslahi ya wananchi wake, kulinda mfumo wa biashara huria na biashara ya pande nyingi, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako