• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • CAF yatoa hukumu kwa Waamuzi waliohusishwa na upangaji matokeo, Watanzania wasafishwa

  (GMT+08:00) 2018-08-03 08:55:28

  Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) limetoa majibu ya uchunguzi wa waamuzi wanne wa Tanzania waliofikishwa kwenye shirikisho hilo, kufuatia kuripotiwa kwa vurugu kwa madai ya kuwa moja ya timu ilitaka kuwapa rushwa waamuzi hao na kupanga matokeo ya mchezo kwenye hoteli waliyofikia nchini Burundi walipokwenda kuchezesha mechi ya ligi ya mabingwa Afrika kati ya Lydia Ludic ya Burundi na Rayon Sports ya Rwanda.

  Katika taarifa yake, CAF imesema waamuzi hao wa Tanzania wako safi na hakuna harufu yoyote ya kupokea hongo kuhusiana na mchezo huo uliochezwa Februari 21 mwaka huu uwanja wa Prince Louis Rwagasore nchini Burundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako