• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuelekea Simba Day: Asante Kotoko ya Ghana kukipiga na Simba Sports Club

    (GMT+08:00) 2018-08-03 08:56:17
    Uongozi wa klabu ya Simba ya Tanzania umetangaza rasmi kucheza na timu ya Asante Kotoko ya Ghana kwenye tamasha lake lijulikanalo Simba Day, Agosti 8 mwaka huu.

    Kupitia Afisa habari wa klabu hiyo Hajji Sunday Manara, amesema, Simba itachuana na timu hiyo kongwe barani Afrika ambayo inashiriki ligi kuu Ghana kwa ajili ya kutambulisha kikosi walichokisajili msimu huu.

    Katika msimamo wa ligi kuu Ghana, Kotoko wamecheza mechi 15 wakiwa kwenye nafasi ya 4 huku wakijikusanyia alama 24 na Ashanti Gold iliyo nafasi ya kwanza ina alama 27 ikiwa imecheza michezo 15 pia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako