• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna mkuu wa UNHCR aitaka Japan kuwatendea haki wahanga wa utumwa wa kingono "haraka"

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:09:10

    Kamishna mkuu wa Shirika la haki za binadamu la Umoja wa mataifa UNHCR Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa mwito kwa serikali ya Japan kuwatendea haki wahanga wa utumwa wa kingono wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia "haraka" iwezekanavyo kwa kuwa wote wamekuwa wazee.

    Bw. Zeid amesema mjini New York kuwa wahanga wa utumwa wa kingono nchini Korea Kusini, Korea Kaskazini na China wanazeeka haraka, na wanahitaji kuona wanatendewa haki kutokana na mateso waliyopata. Pia ameeleza matumaini yake kuwa Japan itarekebisha makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kati yake na Korea Kusini kuhusu suala hilo, ambayo yamepingwa na wahanga na serikali ya sasa ya Korea Kusini.

    Imefahamika kuwa wanawake laki nne barani Asia, nusu yao wakiwa ni wachina, walilazimishwa kuwa watumwa wa kingono kwa jeshi la Japan wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako