• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Walinzi wa amani wa UM warudi kwenye mstari wa utenganishaji kati ya Syria na milima ya Golan

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:09:55

    Kikosi cha Umoja wa mataifa cha Uangalizi wa uwekaji chini silaha UNDOF kimerudi tena kwenye vituo vyake kwenye mstari wa utenganishaji kati ya Syria na milima ya Golan inayokaliwa na Israel, baada ya kuondoka eneo hilo mwaka 2014.

    Shirika la haki za binadamu nchini Syria limesema polisi wa Russia na vikosi vya Syria wametumwa katika mkoa wa Quneitra na kwenye eneo la utenganishaji, baada ya mkoa mzima wa Quneitra kuwa chini ya udhibiti wa serikali.

    Kikosi cha UNDOF kilitumwa mara ya kwanza kwenye eneo kati ya Syria na milima ya Golan mwaka 1974 ili kutenganisha vikosi vya Syria na Israel, baada ya Israel kutwaa udhibiti wa milima ya Golan kwenye vita ya mwaka 1967.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako