• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wastaafu wa Afrika wazitaka nchi za Afrika kutumia majibu ya nyumbani kutatua changamoto

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:19:22

    Viongozi wastaafu wa nchi za Afrika wamewataka viongozi wa sasa na watunga sera kutumia majibu ya nyumbani kutafuta masuluhisho endelevu ya changamoto zinazozikabili nchi za Afrika.

    Akiongea mjini Kigali kwenye mkutano wa tano wa Baraza la uongozi barani Afrika, aliyekuwa Rais wa Msumbiji Bw. Joachim Chissano amesema Afrika ina nafasi nzuri ya kutatua changamoto zake bila uingiliaji wa nje, na inatakiwa kuanza sasa kufanya hivyo.

    Aliyekuwa rais wa Somalia Hassan Mahmoud amewataka viongozi wa nchi za Afrika na watunga sera kuangalia masuluhisho ya ndani, na kuwa na ujasiri wa kutumia masuluhisho hayo kuendana na tamaduni za Afrika.

    Aliyekuwa rais wa Nigeria Olisegun Obasanjo amesema matatizo ya Afrika hayapaswi kulaumiwa kwa wengine, isipokuwa waafrika wenyewe, na nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutoka kwa nchi nyingine za Afrika kupata maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako