• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yahimiza utalii wa mazingira ya asili

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:19:42

    Mtendaji mkuu wa mamlaka ya misitu ya Tanzania Bw. Donsantons Silayo, amesema Tanzania inajipanga kutangaza utalii wa mazingira ya asili, hatua ambayo inatarajiwa kuhimiza sekta ya utalii ya Tanzania, kufungua fursa zaidi za uwekezaji, ambazo pia zitasaidia uhifadhi wa mazingira.

    Bw. Milayo ametolea mfano wa hifadhi ya taifa ya Amani iliyoko katika wilaya ya Muheza kaskazini mwa Tanzania, ambayo amesema ina wanyama na mimea ya pekee, na kusema inafaa kwa utalii wa mazingira ya asili. Tanzania kwa sasa ina misitu 12 ya hifadhi ambayo inamilikiwa na serikali.

    Hata hivyo amesema kuna kazi inayotakiwa kufanywa, ikiwa ni pamoja na kutengeneza barabara za kufika maeneo hayo, na kuwa na malazi kwa ajili ya watalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako