• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini kutokata rufaa kuhusu uamuzi wa mahakama dhidi ya mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-08-03 09:55:40

    Waziri wa mahusiano na ushirikiano wa kimataifa wa Afrika Kusini Bibi Lindiwe Sisulu amesema, serikali ya Afrika Kusini haitakata rufaa kuhusu hukumu ya mahakama ambayo imeweka kando uamuzi wa kutoa kinga ya kidiplomasia kwa Bibi Grace Mugabe mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe kutokana na kesi ya shambulizi.

    Bibi Sisulu pia amesema wamechunguza hukumu hiyo na kufikia makubaliano kuwa hawatakata rufaa.

    Mahakama kuu ya Johannesburg wiki iliyopita ilihukumu kuwa uamuzi uliofanywa na waziri wa mahusiano na ushirikiano wa kimataifa wa zamani Bibi Maite Nkoana-Mashabane wa kutoa kinga ya kidiplomasia kwa Bibi Grace Mugabe, unakiuka katiba na unatakiwa kuwekwa kando.

    Imefahamika kuwa Bibi Mashababe alifanya uamuzi huo Agosti 19 mwaka 2017, baada ya Bibi Grace kudaiwa kuwashambulia mwanamtindo Bibi Gabriella Engels na wanawake wengine wawili huko Johannesburg.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako