• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Emmerson Mnangagwa achaguliwa tena kuwa rais wa Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-08-03 17:06:57

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe Bi Priscilla Chigumba leo ametangaza kuwa, mwenyekiti wa chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF ambaye pia rais wa sasa Bw. Emmerson Mnangagwa amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura na kuchaguliwa tena kuwa rais wa Zimbabwe.

    Bibi Chigumba amesema, "Natangaza kuwa, mwenyekiti wa chama cha ZANU-PF Bw. Emmerson Mnangagwa ameshinda kwenye uchaguzi huo, matokeo hayo ni rasmi kuanzia tarehe 3 Agosti mwaka 2018."

    Takwimu zinaonyesha kuwa, Bw. Mnangagwa amepata kura 2,460,463 katika mikoa 6 kati ya 10, ambayo ni asilimia 50.8 ya kura za jumla. Mpinzani wake mkubwa, ambaye ni kiongozi wa muungano wa upinzani wa MDC Bw. Nelson Chamisa amepata asilimia 44.3 ya kura.

    Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Bw. Mnangagwa amewashukuru Wazimbabwe, na kusema, huo ni mwanzo mpya, na anatumai wote watashirikiana kuijenga Zimbabwe yenye amani, mshikamano na urafiki.

    Wasimamizi wa uchaguzi kutoka nchi za nje, wamesema uchaguzi huo ni muhimu katika historia ya maendeleo ya siasa ya Zimbabwe, na unafungua ukurasa mpya wa Zimbabwe kwa kujipatia ustawi wa uchumi na kuharakisha mchakato wa demokrasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako