• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yawaondolea wananchi wake hofu dhidi ya ugonjwa wa Ebola uliozuka nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-08-04 19:10:25

    Serikali ya Tanzania jana imewaondolea wasiwasi wananchi wake kuhusu kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako watu wanne wamethibitishwa kuwambukizwa.

    Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu ambapo serikali inachukua hatua.

    Waziri amesema serikali itaendelea kutoa elimu ya kujikinga na Ebola pamoja na hatua za kudhibiti ugonjwa huo.

    Aidha waziri huyo amesema makundi ya wataalam yamepata mafunzo na wako tayari kukabiliana na dharura yoyote ya kutokea kwa ugonjwa huo, na tayari vifaa maalum kwa ajili ya kujikinga, na vifaa kwa ajili ya kupimia vimekwishapelekwa kwenye mikoa nane, ikiwemo Dar es Salaam, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma na Kagera.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako