• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua za China za kukabiliana na Marekani ni za kujizuia na zenye unyumbufu

    (GMT+08:00) 2018-08-04 19:22:27

    Kamati ya Ushuru ya Baraza la serikali ya China jana limeamua kuongeza ushuru kwa asilimia 25, 20, 10, na 5 kwa aina tofauti za bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 60. Msemaji wa wizara ya biashara ya China amesema hatua hizo za China ni za kujizuia, na China inabaki na haki yake ya kuendelea kutoa hatua nyingine za kukabiliana kwa kutegemea hatua za Marekani.

    Vita ya biashara haina mshindi, kwa hiyo China inapotoa hatua hizo za kukabiliana, imezingatia maslahi ya wananchi na uvumilivu wa makampuni, na kulinda mzunguko wa uzalishaji kote dunia.

    Kwanza, China haipambani vikali na hatua za Marekani zisizo na maana, bali inashikilia kuzingatia wananchi wake, na kujitahidi kupunguza athari za hatua zinazokabiliana kwa wananchi na makampuni.

    Kwenye orodha ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200, nyingi kati yake hazihusiana na China. Pia ofisi ya wawakilishi wa biashara wa Marekani imeongeza muda wa kutoa maoni kuhusu orodha hiyo hadi tarehe 5 Septemba. Ni dhahiri kwamba, si rahisi kwa Marekani kutekeleza hatua hiyo.

    Pili, lengo la China la kuongeza ushuru wa ngazi nne kwa bidhaa kutoka Marekani ni kupunguza kwa iwezavyo athari ya makampuni ya China na maisha ya wananchi wake, na kuonyesha unyumbufu wa hatua hizo za kukabiliana. Pia ni pigo sahihi linalotolewa baada ya uchambuzi wa athari ya bidhaa kutoka Marekani.

    Kama Marekani itaendelea kutoa shinikizo, China inabaki na haki ya kutoa hatua nyingine za kukabiliana. China ina soko kubwa la ndani, aina zote za viwanda duniani, sera thabiti ya kufungua mlango, hayo yote yanaifanya China iweze kupambana na athari kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako