• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki kuchukua hatua dhidi ya vikwazo kutoka kwa Marekani

    (GMT+08:00) 2018-08-05 17:02:57

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki jana huko Ankara amesema Uturuki itafungia mali za waziri wa utekelezaji wa sheria na waziri wa mambo ya ndani wa Marekani zilizoko nchini humo. Kitendo hicho kimechukuliwa kuwa ni jibu kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Uturuki.

    Rais Erdogan siku hiyo katika mkutano wa chama cha haki na maendeleo cha Uturuki AKP amesema kuwa, haina sababu kwa Marekani kuweka vikwazo dhidi ya Uturuki ambayo ni mwenzi wake wa kimkakati, na Uturuki haitarudi nyuma kutokana na maneno yenye vitisho na uamuzi wa ujinga. Lakini hakutaja majina ya maofisa hao wa Markeani na pia hakuhakikisha kwamba walikuwa na mali nchini Uturuki au la.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako