• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yazionya nchi jirani kujihadhari na mlipuko wa Ebola nchini DRC; AU yashauri juhudi kubwa zifanyike kudhibiti

    (GMT+08:00) 2018-08-05 18:25:43

    Hali mpya ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, imekuwa ni tahadhari kwa nchi za jirani, huku shirika la afya duniani WHO likisema kukabiliana na ugonjwa huo si kazi rahisi.

    Mlipuko mpya wa Ebola wa Agosti 1 nchini DRC, umetokea ikiwa ni wiki moja tangu WHO itangaze kutokomeza mlipuko wa awali Julai 24, na kwamba mlipuko huu mpya uliotokea katika mji wa Kivu hauna uhusiano na mlipuko uliotokomezwa kwenye Jimbo la Ikweta.

    Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi mkuu wa WHO, Peter Salama, zoezi la kupambana ili kuumaliza ugonjwa huo ulitokea tena halitakuwa rahisi katika jimbo la Kivu Kaskazini ambalo ni makazi ya watu zaidi ya milioni 1 waliyojipatia hifadhi baada ya kuyakimbia makazi yao kutokana na vita vya kikabila katika mkoa wa Ituri.

    Hatari nyingine kubwa kwa mujibu wa WHO, ni kuhusu raia wa DRC wanaokimbia vita na kuvuka mpaka kwenye nchi jirani, huku wakiwa wameambukizwa ugonjwa wa Ebola, hivyo shughuli za upimaji na uchunguzi wa kiafya zinafanywa katika sehemu zote za mpakani.

    Nazo mamlaka za afya za nchi jirani za Rwanda, Tanzania na Uganda zimewasihi wananchi kuwa watulivu na kuchukua tahadhari za kujikinga.

    Katika hatua nyingine, Shirika la kudhibiti na Kuzuia Maradhi barani (Africa CDC) limeeleza kuwa, kuna umuhimu wa kuwekwa mkakati imara na ulioratibiwa vizuri ili kukabiliana na ugonjwa wa Ebola uliotokea tena wiki hii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako