• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shanghai kuimarisha hadhi  ya kituo chake cha kifedha cha kimataifa, kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu kwa kupitia kufungua mlango

    (GMT+08:00) 2018-08-05 19:12:14

    Shanghai ni dirisha la kufungua mlango wa mambo ya fedha ya China. Mwaka huu, Shanghai inajitahidi kutekeleza ahadi ya serikali ya China ya kuhimiza zaidi kufungua mlango, na kufanya juhudi katika ushirikiano na kufungua mlango katika sekta ya mambo ya fedha, kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu kwa kupitia kufungua mlango kwa kiwango cha juu.

    Mwaka huu, Shanghai imeweka mpango maalumu, na kuhakikisha mpango na uratibu wa kuijenga Shanghai iwe kituo cha kifedha cha kimataifa. mkurugenzi wa idara ya uchumi wa kitaifa katika kamati ya maendeleo na mageuzi ya Shanghai Bw. Guo Yu amesema, mpaka sasa mpango huo unatekelezwa hatua kwa hatua, na umepata ufanisi mzuri. Shanghai imekuwa na miradi 23 ya majaribio ya kufungua mlango ambayo 9 kati yake yametekelezwa.

    Amesema, kiwango cha kufungua mlango cha mambo ya fedha ni muhimu kwa maendeleo ya Shanghai, Shanghai pia itapanua zaidi kiwango hicho.

    "Kwanza, inapaswa kusukuma mbele zaidi maeneo ya kufungua mlango ya sekta ya mambo ya fedha, ikiwemo shughuli za mabenki, soko la hisa, mambo ya bima, na kufungua mlango na ushirikiano wa ngazi ya juu zaidi kwenye soko la njia kuu za uzalishaji. Pili, ni kuimarisha zaidi maendeleo ya soko la mambo ya fedha la Shanghai na shughuli za mambo ya fedha. Tatu, kutilia maanani zaidi kinga ya hatari ya mambo ya fedha, wakati tunapoendeleza shughuli ya mambo ya fedha."

    Kwa sasa, idara husika zinafanya maandalizi na kusukuma mbele kazi ya kuanzisha utaratibu wa kuunganisha masoko ya hisa ya Shanghai na London ndani ya mwaka huu. Mwishoni mwa mwezi Agosti, idara ya mambo ya fedha ya Shanghai itasaini makubaliano na idara husika za Hongkong na Macao kuhusu kuimarisha maingiliano na ushirikiano wa mambo ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako