• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtoto wa Palestina afariki kwa majeraha aliyopata wakati wa maandamano ya kupambana na Israel katika ukanda wa Gaza.

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:25:22

    Wizara ya Afya ya Gaza imesema mtoto wa Palestina mwenye umri wa miaka 17 amekufa kutokana na majeraha aliyopata wakati wa maandamano ya kupambana na Israel katika mpaka wa Gaza na Israel.

    Msemaji wa wizara hiyo Bw. Ashraf al-Qedra amesema mtoto huyo alipigwa risasi tarehe 30, Machi, siku ya kwanza ya maandamano makuu yanayoendelea ya kurejea ya kuipinga Israel kuizingira Gaza kwa miaka 11.

    Wakati huohuo waandishi wa habari wa Palestina wameandamana katika mlango wa gereza la Ofer cha Israel, magharibi mwa mji wa Ramallah, Ukingo wa Magharibi, wakitaka waandishi wa habari 21 waliofungwa waachiwe.

    Mjumbe wa jumuiya ya wanahabari wa Palestina Bw. Omar Nazzal ameihimiza jumuiya ya kimataifa kubeba majukumu yake katika suala la kuwalinda waandishi wa habari wa Palestina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako