• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahasimu Sudan Kusini wasaini makubaliano ya mwisho kuhusu kuchangia madaraka na usalama

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:34:16

    Pande zinazopambana Sudan Kusini zimesaini makubaliano ya mwisho kuhusu kuchangia madaraka na maswala ya usalama.

    Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Khartoum baada ya upatanishi wa serikali ya Sudan chini ya idhini ya jumuiya ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD. Waliosaini makubaliano hayo ni rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Kiongozi wa kundi kubwa la upinzani Riek Machar na wawakilishi wa makundi mengine ya upinzani.

    Makubaliano hayo yanasema rais wa sasa ataendelea kuwa madarakani katika kipindi cha mpito, na Bw. Machar anarudi kuwa makamu wa kwanza wa rais, na kutakuwa na makamu wengine watatu wa rais kutoka makundi mengine ya upinzani.

    Makubaliano yanasema baraza la mawaziri litakuwa na mawaziri 35, bunge litakuwa na wajumbe 550, 332 kutoka upande wa serikali na 128 kutoka kundi kubwa la upinzani SPLM-IO.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako