• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya inajiandaa kushirikiana na UN kwa ajili ya uchaguzi ujao

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:34:23

    Waziri wa mambo ya ndani wa Libya Bw Abdul Salam Ashour amesema serikali ya Libya inajiandaa kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha uchaguzi wa rais na wabunge unafanyika mwaka huu.

    Mkutano kuhusu suala la Libya ulifanyika mwezi Mei mwaka huu mjini Paris, na pande zote za Libya zilizoshiriki kwenye mkutano huo zilitaka kusimamishwa kwa msukosuko wa kisiasa nchini Libya, na kukubaliana na kuahidi kufanya uchaguzi wa rais na wabunge tarehe 10 mwezi Desemba.

    Mkuu wa baraza la juu la taifa la Libya Khalid al-Meshri ameihimiza serikali ya Libya ifanye mageuzi yanayofaa kwenye sekta za siasa na uchumi. Wakati huo huo, Bunge la mashariki la Libya mbali na mambo ya kisiasa, pia limeuhimiza Umoja wa Mataifa uunge mkono uchumi na usalama nchini Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako