• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magari ya Marekani kuwa mhanga wa kwanza wa vita ya biashara

    (GMT+08:00) 2018-08-06 16:53:53

    Kuanzia Julai 7, bei ya magari ya Ujerumani yaliyotengenezwa nchini Marekani na kuuzwa nchini China imepanda kidhahiri, baada ya China kuongeza kiwango cha ushuru kwa magari hayo kutoka asilimia 15 hadi asilimia 40, hali ambayo imewafanya wafanyakazi wa magari wa Marekani wawe wahanga wa kwanza wa vita ya biashara kati ya China na Marekani.

    Julai 30, kampuni ya BMW ya Ujerumani ilitangaza kupandisha bei ya aina mbili za magari yaliyotengenezwa nchini Marekani na kuuzwa kwenye soko la China kwa asilimia 4 na asilimia 7 mtawalia, kutokana na kuongezeka kwa gharama za vipuri, baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa kutoka nchi nyingi duniani. Wakati huohuo, ikiwa ni moja ya hatua za kulipiza kisasi ushuru wa Marekani, kuanzia Julai 6, China ilianza kutoza ushuru wa asilimia 40 kwa magari yanayoingizwa kutoka Marekani. Hali hiyo inamaanisha kuwa, katika siku zijazo uuzaji wa magari ya chapa mbalimbali yaliyotengenezwa nchini Marekani kwenye soko la China, utapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kupanda bei.

    Kabla ya Marekani kuanza kutoza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa za washirika wake wa biashara, wachambuzi wameona kuwa magari na zana za kielektroniki ambavyo mnyororo wa sekta hizo umekamilika kote duniani, vitaweza kuwa ni wahanga wa kwanza wa vita ya biashara. Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa mwezi Juni na Automotive News ya Marekani, makampuni mia moja makubwa ya kutengeneza vipuri vya magari yako katika nchi 17 zikiwemo Ujerumani, Japan, Canada, Hispania, Korea Kusini, Mexico na China, na utengenezaji wa kila gari lenye vipuri zaidi ya aina elfu kumi hauondokani na ushirikiano na uratibu wa kimataifa kati ya makampuni hayo, ambayo kila moja inachukua nafasi muhimu kwenye mnyororo wa sekta ya magari duniani.

    Gazeti la Financial Times limesema, ili kutimiza ahadi aliyotoa ya kurudisha nafasi za ajira nyumbani, rais Donald Trump wa Marekani alivunja makubaliano ya kimataifa anayodhani yanahujumu maslahi ya wafanyakazi wa Marekani, hatua ambayo ilianza kuyumbisha utaratibu uliopo wa sekta ya magari duniani, na hatimaye wafanyakazi wa Marekani yenyewe watakuwa wahanga wa hatua hiyo.

    Kampuni ya magari ya Daimler ya Ujerumani imesema mwaka jana asilimia 20 ya magari yake yaliyotengenezwa nchini Marekani yaliuzwa kwenye soko la China, na katika robo ya pili ya mwaka huu, faida ya kampuni hiyo ilipungua kwa asilimia 27 kutokana na mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani. Kampuni hiyo pia imesema kama vita hii ya kutozana ushuru kati ya nchi hizo mbili ikiendelea kupamba moto, italazimika kutafakari kupanga upya mfumo wake wa uzalishaji, na kufikiria kujenga kiwanda chake kipya nchini China.

    China ikiwa ni soko kubwa la magari duniani kwa miaka tisa mfululizo, siku zote soko lake linagombewa na makampuni makubwa ya magari ya nchi mbalimbali. Makampuni ya Mercedes Benz na BMW ya Ujerumani yameweka bayana kuwa kama vita ya biashara ikiendelea, yatalazimika kupunguza uzalishaji na wafanyakazi nchini Marekani. Kwa hivyo, sasa ni uamuzi wa Marekani kulinda maslahi ya wafanyakazi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako