• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tarehe ya kuapishwa rais mteule wa Zimbabwe bado haijapangwa

    (GMT+08:00) 2018-08-06 19:51:21

    Msemaji wa ikulu ya Zimbabwe George Charamba amesema, tarehe ya kuapishwa kwa rais mteule Emmerson Mnangagwa itapangwa baada ya serikali kuwa na uhakika kuwa matokeo ya uchaguzi wa Julai 30 hayatapingwa katika mahakama.

    Rais mteule Mnangagwa alishinda uchaguzi wa rais baada ya kupata asilimia 50.8 za kura dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa wa muungano wa MDC aliyepata asilimia 44.3 ya kura.

    Katiba ya Zimbabwe inaelekeza kuwa, mgombea urais ambaye hakuridhika na matokeo anaweza kufungua kesi ndani ya siku saba baada ya matokeo rasmi kutangazwa.

    Wakati huohuo, Umoja wa Afrika (AU) umetaka washirika wote wa kisiasa nchini Zimbabwe kushinda tofauti zao na kushirikiana pamoja kuhakikisha amani, utulivu na maendeleo ya nchi hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vilivyotokea baada ya uchaguzi uliofanyika mwisho wa mwezi uliopita, na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu matukio hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako