• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Baiskeli, Rwanda: Mugisha wa Rwanda ashinda mzunguko wa pili

    (GMT+08:00) 2018-08-07 08:31:43

    Mwendesha baiskeli wa Rwanda Samuel Mugisha amefanikiwa kushinda nafasi ya kwanza kwenye hatua ya pili ya mbio za baiskeli zinazoendelea nchini Rwanda, ambapo alitumia saa 3 dakika 8 na sekunde 56 kwenye umbali wa kilomita 120 kutoka mjini Kigali hadi mji wa kusini wa Huye.

    Nafasi ya pili katika hatua hiyo ilichukuliwa na Uwizeye Jean Claude kutoka Rwanda pia ambaye alitumia saa 3 dakika 9 na sekunde 17. Haile Michael Mulu wa Ethiopia ndiye aliyemaliza mbio za hatua hiyo kwa kushika nafasi ya tatu.

    Mshindi wa hatua ya kwanza Legab Azzedine wa Algeria jana alishindwa kuhimili barabara hiyo yenye vilima na kona nyingi na akishika nafasi ya 5; leo ni zamu ya mzunguko wa tatu ambapo waendesha baiskeli hao watashindana umbali wa kilomita 200, kutoka mji wa Huye hadi Musanze kaskazini ya Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako