• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Man United wakataa ofa ya Barcelona ya fedha pamoja na wachezaji wawili ili kumtoa Pogba

  (GMT+08:00) 2018-08-07 08:32:17

  Klabu ya Manchester United ya Uingereza imekataa ofa nono iliyotolewa na Barcelona ya Hispania kwa ajili ya kumnunua kiungo Paul Pogba wa Ufaransa.

  Barcelona walikuwa tayari kutoa fedha pauni milioni 45 pamoja na wachezaji wao wawili ambao ni Yerry Mina na Andre Gomes kwa ajili ya Pogba, lakini United wakakataa.

  Pamoja na kwamba katika siku za hivi karibuni United walimnyemelea Mina, haikutosha kufumba macho kwani wanadai Pogba ni muhimu zaidi kwao hasa wakati huu.

  Pogba alinunuliwa kwa dau lililoweka rekodi ya dunia la pauni milioni 93.25 akitokea Juventus ya Italia na bado ana miaka mitatu katika mkataba wake na United.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako