• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Msumbiji na Chama cha Renamo wasaini makubaliano kuhusu kupunguza jeshi

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:13:02

    Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ametangaza kuwa serikali yake imesaini makubaliano na chama kikuu cha upinzani Renamo kuhusu kupunguza silaha, kuwapunguza na kuwaingizia kwenye jamii watu wenye silaha wa chama cha Renamo.

    Rais Nyusi ametoa hotuba kwa taifa akisema makubaliano hayo yameonesha wazi mzizi wa masuala ya kijeshi, ambayo ni hatua muhimu inayoweza kutimiza amani ya kudumu, na ameongeza kuwa katika siku kadhaa zijazo watatangaza hatua zijazo juu ya msingi wa makubaliano hayo.

    Pia amehimiza kutumia busara na uvumilivu katika mchakato wa kuwapunguza watu wenye silaha ili kuijenga nchi hiyo iwe na ustawi, uvumilivu na amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako