• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waitaka EAC kuboresha huduma za biashara ili kukuza sekta ya viwanda

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:13:36

    Kamati ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika UNECA imeitaka Jumuiya ya Afrika Mashariki kuifanya biashara iwe huru katika huduma za kitaaluma ili kuhimiza sekta ya uzalishaji viwandani.

    Mkurugenzi wa kitengo cha maendeleo ya uwezo ya UNECA Bw. Stephen Karingi amesema mjini Nairobi kuwa, sekta ya uzalishaji viwandani katika Afrika Mashariki haina ushindani mkubwa kama inavyotakiwa, kutokana na gharama kubwa za huduma katika sekta za bima, sheria, ugavi na fedha.

    Bw. Karingi pia amesema, kuna ushahidi kuwa ufanisi unapatikana wakati masoko yakifunguliwa zaidi. Jumuiya ya EAC itazidi kuhimiza ajenda ya maendeleo ya viwanda kama inaweza kutoa huduma za bei nafuu kutoka soko huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako