• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatangaza mpango wa kukabiliana na dharura kwa Uganda kufuatia mlipuko wa Ebola DRC

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:29:35

    Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza mpango wa kukabiliana na hali ya dharura inayoweza kutokea kwa Uganda baada ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa Ebola kufikia 33 katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    WHO imesema maandalizi ya lazima yamefanywa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hadi Uganda. Mipango imefanywa ili timu ziweze kuchunguza matukio yanayoshukiwa mara moja, huku sampuli zikipelekwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda huko Entebbe, katikati ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako