• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yarejesha vikwazo dhidi ya Iran kwenye sekta zisizo za nishati

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:38:28

    Ikulu ya Marekani imetoa taarifa ikitangaza kurudisha tena vikwazo dhidi ya Iran kwenye sekta zisizo za nishati, zikiwemo fedha, chuma, madini, na magari kuanzia tarehe 7.

    Taarifa pia imesema tarehe 5 Novemba Marekani itarudisha tena vikwazo kwenye mambo mengine yanayosalia, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kuendesha bandari ya Iran, sekta za nishati, usafirishaji baharini na utengenezaji wa meli, biashara ya mafuta, biashara kati ya mashirika ya fedha ya nchi za nje na benki kuu ya Iran.

    Wakati huo huo, rais Hassan Rouhani wa Iran amesema wananchi wa Iran wataifanya Marekani ijute kutokana na kurejesha vikwazo dhidi ya nchi yao.

    Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa kanuni mpya ya kujibu vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran itaanza kufanya kazi leo, ili kulinda maslahi ya watu na makampuni ya Umoja huo. Kwa mujibu wa kanuni hiyo, bila idhini ya kamati ya Umoja wa Ulaya, watu na makampuni ya Umoja wa Ulaya hawaruhusiwi kufuata kanuni zilizowekwa na vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako