• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande husika zatoa maoni kuhusu makubaliano ya amani ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-08-07 09:59:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying amesema kutokana na upatanishi wa jumuiya ya kimataifa, hasa Sudan na shirika la IGAD, pande hasimu za Sudan Kusini zimesaini makubaliano ya amani huko Khartoum, na China inapongeza hatua hii muhimu ya kuhimiza mchakato wa amani ya Sudan Kusini.

    Amesema China inatarajia kwamba pande husika zitatekeleza mapema makubaliano hayo na kurejesha amani na utulivu wa Sudan Kusini. China itatoa msaada kwa mchakato wa amani wa Sudan Kusini kadiri ya uwezo wake.

    Kwa upande mwingine, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amekaribisha kusainiwa kwa makubaliano hayo. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaiunga mkono IGAD na Umoja wa Afrika, ili kufikia makubaliano ya amani, ya haki na ya kudumu kwa Wasudan Kusini.

    Wakati huohuo katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Bw. Aboul-Gheit alieleza matumaini yake kwamba makubaliano hayo yatakomesha mgawanyiko na vita ya miaka mitano huko Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako