• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yamrejesha raia wa Korea Kusini kupitia kijiji cha Panmunjom

    (GMT+08:00) 2018-08-07 17:13:05

    Korea Kaskazini leo imemrejesha kwao raia wa Korea Kusini kupitia kijiji cha mpakani cha Panmunjom.

    Jana, Shirika la Msalaba Mwekundu la Korea Kaskazini lilitoa taarifa kwa Korea Kusini kuhusu mpango wa kumrejesha raia huyo, ambaye alikamatwa Julai 22 baada ya kuingia isivyo halali nchini Korea Kaskazini.

    Hatua hiyo imekuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukiboreka zaidi baada ya rais Moon Jae-in wa Korea Kusini na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un kufanya mkutano wao wa kwanza huko Panmunjom April 27 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako