Polisi nchini Zimbabwe wanawasaka viongozi wanane wa ngazi ya juu wa muungano wa upinzani wa MDC kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wiki iliyopita mjini Harare zilizosababisha vifo vya watu sita na wengine saba kujeruhiwa.
Mpaka sasa watu 27 wamekamatwa kufuatia vurugu zilizotokana na maandamano, na watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani hii leo.
Wakati huohuo, muungano wa upinzani MDC ambao unapinga matokeo ya uchaguzi, unadai kuwa mamlaka nchini Zimbabwe zimeongeza msako dhidi ya viongozi na wafuasi wake baada ya uchaguzi uliofanyika Julai 30 ambapo rais wa sasa wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa na chama chake cha ZANU-PF kimepata ushindi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |