• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Kampuni za Australi na Uingereza kujenga bomba la Uganda-Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-08-07 19:40:26

  Kampuni ya WorleyParsons kutoka Australia na ile ya Penspen kutoka Uingereza zinashindania kupata zabuni ya kujenga bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

  Hata hivyo duri zinaarifu kuwa huenda kampuni zote mbili zikapewa zabuni hiyo ya kutekeleza uhadisi, ununuzi na ujenzi wa bomba hilo.

  Katibu wa kudumu katika wizara ya kawi nchini Ugand Robert Kasande amesema makubaliano kati ya serikali na kampuni za Tullow Oil, Total na China National Offshore Oil ambazo zinachimba mafuta kwenye eneo la Hoima huenda yakasainiwa ndani ya miezi mitatu ijayo.

  Tanzania na Uganda zitagharamia asilimia 70 ya ujenzi wa bomba hilo kupitia washirika wao wa kifedha huku asilimia 30 ikigharamiwa na Total, Tullow, CNOOC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako