• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wafanyakazi wa benki wasio waadilifu kuchukuliwa hatua

  (GMT+08:00) 2018-08-07 19:40:48

  Waziri wa Fedha na Mipango, wa Tanzania Dk Philip Mpango ameziagiza benki zote nchini kuanza mchakato wa kuwachunguza na kuwachukulia hatua mbalimbali zikiwamo za kuwafukuza kazi, wafanyakazi wasio waadilifu ili kukomesha matukio ya wizi wa fedha za wateja katika benki.

  Ameahidi kuzichukulia hatua benki zote ambazo hazitafanya uchunguzi huo kwa sababu Serikali imekusudia kukomesha wizi katika benki ili kuhakikisha fedha za wananchi zinakuwa salama.

  Dk Mpango ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa tawi la benki ya Amana jijini Tanga akimuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika uzinduzi huo.

  Dk Mpango amesema katika baadhi ya benki nchini kuna watumishi wanafanya vitendo vya wizi wa fedha za wateja wao kwa kutumia njia mbalimbali zikiwamo za mitandao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako