• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wazalishaji wa bidhaa watakiwa kuthibitishwa ubora wake

  (GMT+08:00) 2018-08-07 19:42:13

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa miezi mitatu kwa wazalishaji wa bidhaa zilizo katika orodha ya viwango vya lazima kutakiwa kuthibitishwa ubora wake.

  Katika kipindi hicho, shirika litathibitisha ubora wa bidhaa hizo na wasambazaji na wauzaji watatakiwa kuingiza sokoni bidhaa zenye ubora.

  Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Ngenya Yusuf alitoa agizo hilo katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu katika uwanja wa Nyakabindi.

  Alifafanua kuwa bidhaa zilizo katika viwango vya lazima ni zile zinazoweza kuleta athari za kiafya, kiusalama ama kuharibu mazingira.

  Alitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na bidhaa za vyakula, vifaa vya ujenzi, vilainishi vya mitambo na bidhaa za petroli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako