• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN aendelea kuunga mkono makubaliano ya nyuklia baada ya Trump kurejesha vikwazo dhidi ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-08-08 09:28:29

    Baada ya rais Donald Trump wa Marekani kutangaza Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema uhusiano kati ya pande mbili ni maamuzi ya nchi husika, na Umoja wa Mataifa hautaki kuingilia sera za ndani ya nchi.

    Msemaji huyo amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa Makubaliano hayo yanayojulikana kama JCPOA, ambayo pande zote zinapaswa kuyaunga mkono na kuyafuata kwa makini.

    Wakati huohuo, wizara ya mambo ya nje ya Russia imetoa taarifa ikisema Russia italinda ushirikiano wa kiuchumi na wa kibiashara na Iran, na kufanya juhudi za kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw Heiko Josef Maas amewaambia wanahabari kuwa Ujerumani na Umoja wa Ulaya watafanya juhudi kudumisha uhusiano wa kiuchumi na kibiasahra na Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako