• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini DRC wamefikia 16

    (GMT+08:00) 2018-08-08 09:33:24

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani WHO, hadi kufikia Agosti 6, idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuambukiziwa virusi vya Ebola nchini DRC imefikia 16 na wengine 27 wanashukiwa kuambukizwa na virusi hivyo, 34 kati yao wakiwa wamefariki dunia. Hivi sasa Shirika hilo linashirikiana na pande mbalimbal kufanya juhudi za kudhibiti maambukizi hayo.

    Habari nyingine zinasema waziri wa afya wa Rwanda Bibi Diane Gashumba amewataka mameneja wa hoteli na kampuni za uchukuzi kuwa mstari wa mbele, na sehemu ya mkakati wa kukinga maambukizi ya Ebola.

    Bibi Gashumba amekutana na viongozi wa dini, wamiliki wa hoteli na kampuni za uchukuzi huko Kigali, na kuwaarifu kuhusu maendeleo ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini DRC na hatua za udhibiti na maandalizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako