• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikapu, Michuano ya Afrika chini ya Miaka 18 Wanawake: Uganda wawasili Msumbiji

  (GMT+08:00) 2018-08-08 09:43:24

  Timu ya taifa ya Uganda ya vijana chini ya umri wa miaka 18 wanawake ya mchezo wa mpira wa kikapu, jana imesafiri hadi nchini Msumbiji ambako inakwenda kushiriki michuano ya Afrika.

  Uganda ambayo ilifuzu mashindano hayo baada ya kuibuka mshindi wa pili katika michuano ya ukanda wa Afrika, ina jumla ya wachezaji 12 ambao wote ni wanafunzi wa shule za sekondari.

  Kwa mujibu wa kocha mkuu Ali Mavita, timu hiyo imefanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo licha ya kukabiliwa na ufinyu wa nafasi na muda kwa kuwa wengi wa wachezaji walikuwa wanakabiliwa na masomo.

  Kwenye mashindano hayo ya Afrika yanayoanza Agosti 10 hadi Agosti 19, Uganda itachuana na timu kutoka nchi za Msumbiji, Misri, Rwanda, Madagascar, Tunisia na Angola.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako