• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mbio za Baiskeli, Rwanda: Hellmann wa Ujerumani ashinda hatua ya 3, Mugisha wa Rwanda aongoza kwa takwimu za jumla

  (GMT+08:00) 2018-08-08 09:43:47
  Katika siku ya tatu ya mbio za baiskeli nchini Rwanda jana, Julian Hellmann wa kutoka ujerumani alifanikiwa kushinda katika hatua ya tatu yenye umbali wa kilomita 200 kutoka mjini Huye hadi Musanze akitumia saa 5 dakika 11 na sekunde 4.

  Nafasi ya pili ilikwenda kwa David Lonzano wa Hispania, nafasi ya tatu ikienda kwa Calvin Beneke wa Afrika Kusini, na bingwa wa mashindano kama hayo msimu uliopita Valens Ndayisenga wa Rwanda jana alikamata nafasi ya tano.

  Katika takwimu za jumla kwenye hatua tatu ya mbio hizo zilizopita Samuel Mugisha wa Rwanda anaongoza kwa kuwa ndiye aliyerekodi muda mfupi zaidi, akiandika saa 10 na dakika 34 pekee katika umbali wa kilomita 420.

  Mbio hizo zinaendelea tena leo, ambapo waendesha baiskeli hao watashindana katika umbali wa kilomita 136 kuanzia mji wa Musanze hadi Karongi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako