• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Golikipa Essam El-Hadary astaafu kuitumikia timu ya taifa ya Misri

  (GMT+08:00) 2018-08-08 09:44:22

  Hatimaye golikipa wa kimataifa wa Misri Essam El-Hadary jana ametangaza kustaafu kutumikia timu ya taifa ikiwa ni baada ya kuitumikia kwa miaka 22, akiwa amecheza mechi 159.

  Kipa huyo ambaye mwaka huu ameandika rekodi ya dunia kwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kushiriki michuano ya kombe la dunia, kwani alikuwa na miaka 45 na siku 161 wakati wa michuano ya mwaka huu.

  El-Hadary ambaye mpaka sasa ni mchezaji wa klabu ya Ismailia inayoshiriki ligi kuu nchini Misri amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na mafanikio aliyopata akiwa na timu ya taifa pamoja na klabu 10 alizocheza mpaka sasa.

  Miongoni mwa mafanikio aliyoyapata, El-Hadary ameshinda ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika mara 4, na ubingwa wa nchi za kiarabu mara 1 akiwa na timu ya taifa ya Misri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako