• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shughuli za China za ulinzi wa wanyamapori zapongezwa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-08-08 10:12:26

    Juhudi za China za ulinzi wa wanyamapori zimepongezwa kwenye sherehe za utoaji tuzo za ulinzi wa wanyamapori barani Afrika zilizofanyika Cape Town, nchini Afrika Kusini. Tuzo hizi zilizoanzishwa kwa pamoja na kampuni za Alibaba na Mfuko wa Paradise wa China.

    Kupitia mpango wa makampuni hayo mawili, walinzi wa wanyamapori wapatao 50 barani Afrika, hupewa tuzo ya dola elfu 3 za Marekani kila mwaka kwa miaka 10 mfululizo, kutambua mchango wao kwenye ulinzi wa wanyamapori.

    Baadhi ya mambo muhimu yaliyotajwa kwenye sherehe hizo ni mchango muhimu wa China kwa kushirikisha ulinzi wa mazingira, uvumbuzi na teknolojia.

    Akiongea kwenye sherehe hizo mkubwa wa kampuni ya Alibaba na mwenyekiti mwenza wa mfumo wa Paradise Bw. Jack Ma, amesema watahimiza mwamko wa ulinzi wa wanyamapori barani Afrika kwa watu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako