• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya alisaidia shirikisho la wakuu wa shule kupata hadhi ya mwangalizi

    (GMT+08:00) 2018-08-08 10:12:53

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ataliombea shirikisho la wakuu wa shule hadhi ya mwangalizi kwenye Umoja wa Afrika.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa 10 wa wakuu wa shule za nchi za Afrika uliofanyika mjini Mombasa, Rais Kenyatta amesema atafanya hivyo ili kulipa shirikisho hilo nafasi ya uongozi katika mambo ya Afrika.

    Amewapongeza walimu na kusema wao ndio wanawafundisha watoto wa vizazi vipya vya Afrika kuhusu umoja wa waafrika. Hata hivyo Rais Kenyatta ametoa changamoto kwa Shirikisho hilo, kuhakikisha kuwa linakuwa na wanachama kutoka nchi zote za Afrika kabla ya kupata nafasi ya mwangalizi kwenye UImoja wa Afrika.

    Kenya inapanga kuchukua uenyekiti wa shirikisho la walimu wakuu wa shule, na kuomba nafasi ya uenyeji wa mkutano huo kwa mwaka 2021.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako