Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu OCHA imesema nishati za dharura zinazotumiwa kwa ajili ya vifaa vya matibabu na maji katika ukanda wa Gaza zinakaribia kwisha na kufanya watu kuwa na umeme kwa muda usiozidi saa 4 kila siku. Ofisi hiyo imekadiria kuwa lita elfu 60 za nishati za dharura zinapaswa kusambazwa ili kuhakikisha vifaa hivyo vinatoa huduma katika siku nne zijazo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |