• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yapongezwa kwa kusaini makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2018-08-08 18:34:23

    Tume ya Pamoja ya Usimamizi na Tathmini (JMEC) imezipongeza pande zinazopingana nchini Sudan Kusini kwa kusaini makubaliano ya mwisho ya amani katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na kutoa wito wa utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo mjini Juba imesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kumeongeza nguvu ya uhai kwa Makubaliano ya Kusuluhisha Mgogoro wa Sudan Kusini ya mwaka 2015, na yanatarajiwa kutimiza amani ya kina na jumuishi, kurejesha usalama, utulivu na kuboresha upatanishi wa kitaifa nchini Sudan Kusini.

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa upinzani Riek Machar wa chama cha SPLM-IO na makundi mengine ya upinzani walisaini makubaliano yaliyoratibiwa na rais Omar al-Bashir wa Sudan chini ya shirika la kikanda la IGAD. Katika makubaliano hayo, Machar atarejea kwenye nafasi yake ya Makamu wa kwanza wa rais, na makamu rais wengine wanne watateuliwa katika serikali ya mpito ya umoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako