• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Wafanyabiashara wa chai wapata pigo vya biashara vya Marekani dhidi ya Iran

  (GMT+08:00) 2018-08-08 19:27:50

  Chama cha wafanyabiashara wa chai Afrika Mashariki (Eatta) kimeitaka serikali ya Kenya kuingilia kati ili kudumisha mauzo ya chai nchini Iran wakati vikwazo vya kibiashara vya Marekani vilianza kutekelezwa jana.

  Marekani imelazimisha tena vikwazo vya kibiashara dhidi ya Iran,na kurejesha tena adhabu kali zilizoondolewa mwaka 2015.

  Aidha Marekani imetoa onyo kwamba itaziwekea vikwazo nchi zitakazoendelea kushirikiana kibiashara na Tehran.

  Iran ni mojawapo ya wanunuzi wa jadi wa chai ya Kenya ,na katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi Juni ilinunua bidhaa za gharama ya Sh575 milioni.

  Mkurugenzi Mkuu wa Eatta Edward Mudibo amesema wanataka kuzungumza na serikali na wadau wengine ili kuangalia chaguo ambalo wanaweza kukumbatia wakati huu wa vikwazo vya kibiashara.

  Mudibo alisema serikali,kupitia Benki Kuu ya Kenya (CBK),inafaa kuingilia kati na kuwasaidia wafanyabiashara kupata malipo yao kwa wakati ufaao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako