• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Vita vya kung'ang'ania umiliki wa soko la anga ya Tanzania vyapamba moto

  (GMT+08:00) 2018-08-08 19:28:52

  Vita vya kibiashara kwa ajili ya anga ya Tanzania vimeanza wakati mashirika ya ndani ya ndege yakipunguza nauli na kuanzisha promosheni mbalimbali katika wimbi la ushindani mkali.

  Haya yamejiri baada ya ripoti kwamba umiliki wa soko la ndani wa Shirika la Ndege la Air Tanzania umeongezeka hadi asilimia 20 kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 wakati ilipoanza tena safari yake ya ufufuo.

  Umiliki wa soko wa shirika la ndege la Fastjet ulikuwa asilimia 42 katika robo ya kwanza ya mwaka huu wakati kampuni ya Precision Air ilikuwa na umiliki wa kati ya asilimia 30 na 40 wa soko..

  Precision Air imepunguza nauli ya safari moja ya njia ya Dar-Kilimanjaro kutoka Sh230,000 hadi 150,000 kuanzia Julai 13 hadi Desemba 31.

  Fastjet nayo jana ilitangaza ofay a vinywaji vya bure na mizigo kutolipishwa hadi kilo 23 kwa kila msafiri kwa tiketi ambazo zitanunuliwa kuanzia tarehe 6 Agosti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako