• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Benki zatenga fedha kwa ajili ya mikopo katika sekta ya mafuta na gesi

  (GMT+08:00) 2018-08-08 19:30:29

  Benki za Uganda zinaendelea kuvutiwa na sekta ya mafuta na gesi nchini Uganda.

  Wiki tatu zilizopita,Benki ya Barclays,ambayo sasa inajulikana kama Absa,imeelezea nia yake ya kutumia fursa katika sekta ya mafuta na gesi.

  Hatua hii ni sehemu ya mpango mkubwa wa benki hiyo kukua na kuongeza faida.

  Benki ya hivi karibuni kupiga hatua hiyo ni Benki ya Equity,ambayo imesema kuwa imetenga zaidi ya $250m kwa ajili ya mikopo kwa watu binafsi na makampuni yenye nia ya kuwekeza katika sekta ya mafuta na gesi.

  Benki ya Equity inafanya oparesheni zake katika nchi sita barani Afrika na ina mtaji wa takriban $1b.

  Katika kikao na waandishi wa habari wakati wa kusherehekea miaka 10 ya benki ya Equity nchini Uganda,Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo James Mwangi alisema benki hiyo sasa inaweza kutoa mkopo wa hadi $250m kwa mtu binafsi au watu wengi zaidi ambao wana mpango mzuri wa biashara katika sekta ya mafuta na gesi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako