• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda-AGRF kutazama njia za kupunguza uagizaji chakula Afrika.

  (GMT+08:00) 2018-08-08 19:30:49

  Rwanda ainatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano la Mapinduzi ya Kilimo la mwaka 2018 (AGRF) mwezi ujao kujadili kuhusu matatizo yanayowapatia changamoto wakulima wadogo kufuatia ripoti kwamba bara la Afrika linatumia mabilioni ya dola za Marekani kuagiza chakula kila mwaka.

  Kulingana na takwimu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),bara la Afrika linatumia $35b kuagiza chakula kila mwaka.

  Takwimu hizo zinatarajiwa kuongezeka $110b kufikia mwaka 2025 ikiwa mwenendo huu hautabadilika.

  Kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), wakulima wadogo huzalisha asilimia 80 ya chakula katika nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara na Asia,na uwekezaji wa kuboresha uzalishaji wao unahitajika haraka.

  Wataalamu wa FAO wanasema kwamba,katika nchi nyingi,upatikanaji wa uvumbuzi,teknolojia na habari ni mchache kwa wakulima wadogo,pamoja na pembejo na mbegu za hali ya juu za kuboresha uzalishaji na mapato.

  Kongamano hilo ambalo litafanyika kuanzia tarehe 5-8 Septemba mjini Kigali linalenga kuwawezesha wakulima wadogo kukabiliana na uhaba wa chakula barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako