• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Kocha wa timu ya taifa U-17 anamatumaini ya kikosi chake kitatinga fainali

  (GMT+08:00) 2018-08-09 08:48:38
  Kocha wa timu ya taifa ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 wa Kenya, Mike Amenga amesema kikosi hicho kina uwezo mkubwa wa kufuzu fainali za Afrika za 2019.

  Amenga amesema hayo kabla ya kuondoka na timu hiyo kuelekea Tanzania kwa mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na (CECAFA).

  Katika mashindano ya CECAFA ambayo yataanza Agosti 11 hadi Agosti 26 katika uwanja wa kitaifa jijini Dar es Salaam, Kenya imepangiwa kuanza na Sudan Kusini hapo Agosti 14.

  Wakati huo huo, Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye amezitaka timu zote kuhakikisha zinawakilishwa na wachezaji walio na umri unaofaa, la si hivyo zitaadhibiwa vikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako