• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatafuta ushirikiano na sekta binafsi ili kutoa huduma za afya kwa wote

    (GMT+08:00) 2018-08-09 09:16:50

    Wizara ya afya ya Kenya itaanzisha ushirikiano wa kimkakati na sekta binafsi, ili kupanua upatikanaji wa huduma za afya zilizo bora na za gharama nafuu. Waziri wa afya wa Kenya Bibi Sicily Kariuki, amesema ushiriki wa sekta binafsi wenye nguvu utawezesha serikali ya Kenya kutimiza moja ya ajenda nne kubwa kuhusu afya kwa wote kabla ya mwaka 2022.

    Bibi Kariuki ameongeza kuwa serikali ya Kenya iko tayari kukusanya raslimali kutoka sekta binafsi kuhimiza utafiti wa kibaiolojia na kutoa mafunzo ya kiwango cha juu kwa watumishi adimu wa afya, kama wa tiba za uvimbe na mionzi

    Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda cha Kenya Bw Kiprono Kittony, amesema uwekezaji wa sekta binafsi kwenye maeneo ya miundo mbinu, uzalishaji viwandani na kutoka mafunzo kwa wahudumu wa afya, kutahimiza juhudi za serikali kukabiliana na ongezeko la gharama za matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako